Ni muendelezo wa msimu mbaya kwa kiungo wa Man United na timu ya Taifa ya Uholanzi, Donny Van De Beek. Majeruhi kumkosesha nafasi ya kucheza Euro 2020.

Van De Beek alijiunga na United mwezi Agosti 2020 akitokea Ajax. Usajili wa Donny haukutegemewa na wadau wengi wa soka hasa mashabiki wa United na mpaka msimu wa 2020/21 unahitimishwa, Donny Van De Beek alikuwa ni mchezaji asiye na namba kwenye kikosi cha kwanza cha Ole Gunnar Solskjaer.

Pengine mashindano ya Euro 2020 ndio ilikuwa sehemu ya Van De Beek kuonesha uwezo wake wa kucheza soka la kiufundi lakini mambo yamekuwa tofauti. Kocha wa Timu ya Taifa ya Uholanzi, Frank De Boer amethibitisha kuondolewa kwa mchezaji huyo kwenye kikosi cha timu yake na hana mpango wa kuweka mchezaji wa mbadala kwenye nafasi hiyo.

Van De Beek alikuwa kwenye benchi kwenye mchezo dhidi ya Scotland licha ya kutokuwepo kwenye mazoezi ya timu hiyo sambamba na wachezaji wengine. Kwa upande wa United, ni imani ya benchi la ufundi kuwa Donny atapona haraka kuelekea kwenye maandalizi ya msimu ujao 2021/22.


WEKA PESA KUPITIA DUKANI MERIDIANBET!

Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.

Weka Pesa Meridianbet

WEKA PESA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa