Fraga Bado Ana Nafasi Ya Kung'aa Simba

Huku tetesi nyingi za usajili zikiendelea kwenye ligi kuu bara, Msimbazi kuna sitofahamu kubwa kuhusu nafasi ya viungo wakabaji wa timu hiyo, Gerson Fraga anahusishwa kurudi Msimbazi huku Jonas Mkude akiendelea kupuyanga!

Bado Simba inamuhitaji Gerson Fraga ndani ya timu, hii inaweza kuongeza ubora na upana wa kikosi chao. Fraga aling’aa sana na Simba wakati wa mechi za mwanzo mwa msimu kabla ya kupata majeraha!

Fraga

Baada ya mbrazil huyo kupata majeraha, Simba ilimsajili Lwanga ambaye anacheza vizuri sana na uwepo wake unahakikisha usalama katika safu ya ulinzi ya Simba.

Kwa bahati mbaya sana, Simba ina Thadeo mmoja tu, yani mmoja, unajiuliza kuhusu Jonas Mkude?

Ni hivi, ndani ya Thadeo kuna Jonas Mkude na ndani ya Mkude hakuna Thadeo Lwanga, ndani ya Thadeo kuna Gerson Fraga na ndani ya Fraga kuna Thadeo Lwanga.

Kiasili Mkude si kiungo anaeweza kucheza katika mazingira ambayo timu inazuia zaidi (kiungo wa ulinzi), huyu ni mtu ambae atakupa uhatari wake pale ambapo Simba inamiliki mpira kuliko mpinzani.

Katika soka la kisasa kuna aina nyingi za viungo ikiwemo Defensive Midfielder na Holding Midfielder, hawa wote ni viungo wa chini lakini wanatofautiana majukumu ndani ya Uwanja.

Holding Midfielder ni kiungo ambae anazuia nafasi baina ya viungo washambuliaji na walinzi wanaocheza nyuma yake na si mzuri sana katika kuzuia badala yake atakupa ubora katika kupiga pasi ndefu au fupi kutokea katika mzizi wa eneo la kiungo, Mkude anaingia hapa.

fraga na mkude

Defensive Midfielder hawa wanafanya kazi chafu na muda mwingi hucheza ndani ya mita 20 katika eneo lao, ni viungo ambao wanaweza kucheza kama walinzi wa kati na akili yao ipo katika kuzuia zaidi.

Defensive Midfielder huku mtaani tunawaita wavunja kuni, hawa wanafurahia zaidi kukaba kuliko kitu chochote ndani ya Kiwanja, Fraga na Lwanga wanaingia hapa.

Si dhambi kuwa na Lwanga, Gerson na Mkude kwa wakati mmoja, unatengeneza ushindani wa namba na ubora wa kikosi. Tusubiri kuona kurejea kwake kutaleta matunda gani msimbazi kama Simba itaona ulazima wake!


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

2 Komentara

    Fraga yupo vizuri bado nafasi ipo

    Jibu

    Fraga jembe

    Jibu

Acha ujumbe