UEFA na FIFA wamepanga kwenda mahakamani wiki ijayo kwa ajiri kwa kutafuta usaidizi wa kiseheria kwa ajiri ya kuzuia mashindano ya Super League kutokufanyika ili kuweza kuzuia baadhi vilabu kuachana na mpango huo kabisa.

Mgogoro kati ya UEFA, FIFA na Waanzilishi wa mashindano ya Super League umetokona na kiasi kikubwa cha fedha kitakachotumika kwenye mashindano hayo, ambapo mashirikisho hayo yameogopa kutengenezwa matawi kwa michezo mingine, huku makampuni makubwa yakiahidi kuwekeza pesa nyingi zaidi kwenye mashindani hayo.

Super League, Super League Kuamuliwa Mahakamani, Meridianbet

Baada ya mashindano hayo kutangazwa mwezi April mwaka jana, yalikufa ndani ya saa 48 tu baada ya kutangazwa kwake, kutokana na kupingwa vikali na mashabiki, taasisi za serikali, bodi mbalimbali za ligi na baadhi ya wachezaji .

Baada sekeseke la kupinga mashindano hayo bodi za ligi za nchi kadhaa ambazo zinatoa  timu shiriki, zilitishia kuziondioa timu hizo, endapo zitaendelea kushiriki michuano ya Super League, vilabu vya Manchester United, Liverpool, Manchester City, Chelsea, Tottenham Hotspur, Arsenal, AC Milan, Inter Milan and Atletico Madrid vilijiondoa.

Mpaka sasa ni klabu tatu tu ndio zimebaki na msimamo wa kutaka kuendelea na mashidano ya Super League, vilabu hivyo ni Real Madrid, Juventus na Barcelona.

Mahakama inatarajiwa kuamua kama mashindano hayo yana athari kwa mashirikisho hayo na haki ya kuwazuia wachezaji na timu kushiriki michuano ya Super League.


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa