Inavyoonekana, Everton hawatotangaza kocha mpya kabla ya wiki ijayo. Tangu kuondoka kwa Carlo Ancelotti, vigogo wa klabu hiyo wanahaha kumpata mbadala wake.

Ancelotti aliondoka Goodison Park na kutimkia Bernabeu ambapo kwake ni amerudi nyumbani, msimu ujao atakua akiiongoza Real Madrid.

Alipotoka, uongozi wa klabu [Everton] unahaha katika mchakato wa kuamua nani anafaa kuchukua mikoba ya Ancelotti. Takribani makocha 8 wanahusishwa na klabu hiyo na baadhi yao wameshafanya mazungumzo ya awali katika mchakato wa kukabidhiwa kibarua hicho.

Rafael Benitez, Nuno Espirito Santo, Duncan Ferguson, Eddie Howe, Christophe Galtier na Roberto Martinez. Ijapokuwa, mashabiki wa klabu hiyo wanapinga uwezekano wa Benitez kupewa timu hiyo, inasemekana Farhad Moshiri anamuhusudu zaidi kocha huyo kuliko wengine na huenda akawashangaza mashabiki wa klabu hiyo.


SHINDA TSH 150,000,000/=

Mtaani kumechangamka, washkaji wanakamata mkwanja kwa mkakati tu na Footbal Fever! Ni rahisi, changamkia fursa hii kushinda mgao wako wa TSH 150,000,000/= 💰🤑

Atletico, Atletico Waunga Tela kwa Calhanoglu, MeridianbetINGIA MCHEZONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa