Kunako mchezo wa mbio za langalanga [F1], kalenda ya mbio za 2020/21 imebadilika kutokana na maambukizi ya COVID19. Uturuki kuchukua nafasi ya Canada.

Kwa mujibu wa kalenda ya awali ya F1, mbio za Canadian Grand Prix, zilipangwa kuchezwa Juni 11-13. Kutokana na muenendo wa maambukizi ya COVID19 na taratibu za kujilinda na ugonjwa huu, Turkish GP itakuwa mbadala wa Canadian GP.

Huu ni mwaka wa pili mfululizo, mbio za Canada zinasitishwa kutokana na maambukizi ya COVID19. Vikwazo vya kiusafiri vimekuwa kikwazo kwani zinahitaji wasafiri kukaa karantini kwa siku 14.

Japokuwa, mkataba wa F1 kuchezwa Gilles Villeneuve, Montreal-Canada umeongezwa kwa miaka miwili mpaka 2031. Uturuki wanarejea kwa mara ya pili mfululizo mwaka huu kama sehemu iliyokuwa imetayarishwa kutokana na hali ya COVID19 inavyoendelea sehemu mbalimbali duniani.

F1, F1: Turkish GP Mbadala wa Canadian GP., Meridianbet
Mara ya mwisho mbio za Canadian GP kufanyika Montreal ilikuwa 2019.

Mwaka jana, Turkish GP ilifanyika kwa mara ya kwanza tangu 2011. Kurejea kwa mbio hizo zilikuwa neema kwa Lewis Hamilton ambaye aliifikia rekodi ya dunia kwa kubeba taji lake la 7 kupitia ushindi alioupata kwenye mbio hizo.

Raisi wa Formula 1, Stefano Domenicali amesema “Japokuwa tunahuzunika kuwa hatutoenda Canada msimu huu, tunafurahi kuthibitisha Uturuki watasimamia mbio za 2021 baada ya kufanya vizuri mwaka jana.

“Ninapenda kuwashukuru mapromota na mamlaka za Canada kwa kujitahidi kadiri walivyoweza kwa wiki kadhaa zilizopita, lakini vikwazo vya usafiri zimekwamisha mipango yetu.”


KWANI MERIDIANBET WANASEMAJE! MKWANJA UPO KWENYE KASINO MPYA YA MINI POWER ROULETTE.

Unawezaje kukosa ubingwa ndani ya kasino hii maridhawa, Nafasi ya kushinda mkwanja ni kwa kila mtu, Meridianbet inakupa nafasi ya kuwa mmoja ya washidi leo, unasubiri nini?

Mini Power Roullete

CHEZA HAPA

3 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa