Chelsea na Vita ya Kuuza Tiketi za Mchezo wa FA Cup

Mashabiki wa Chelsea hawapaswi kuadhibiwa na vikazo vya mmiliki wa klabu hiyo na wanapaswa kuruhusiwa kununua tiketi za mchezo wa nusu fainali ya FA Cup dhidi ya Crystal Palace mwezi ujao, mwenyekiti wa bunge la Uingereza leo Jumatatu.

Klabu ya Chelsea inaendeshwa kwa vibali maalum kutokana na serikali ya nchini Uingereza kuiwekea vikwazo klabu hiyo na mali zote ambazo zinamilikiwa na mmiliki wa klabu hiyo ambaye anahusishwa kuwa na uhusiano wa moja kwa moja na rais wa Urusi.

Chelsea

Kibali kilichotolewa na serikali inaruhusu klabu hiyo kumalizia michezo yake na kulipa mishahara ya waajiriwa wake lakini inazuia klabu hiyo kuuza tiketi na kufanya biashara yeyote, tiketi zinaweza uzwa ikiwa, marekebisho ya kibali chao kufanyiwa marekebisho.

“Ni ajabu sana kutarajia kuona nusu uwanja kwenye uwanja wa Wembley kwenye mchezo wa nusu fainali ya FA Cup kati ya Chelsea na Palace.” Alisema Knight, mwenyekiti wa michezo, sanaa na habari.

“The Blues ni zaidi ya mmiliki, ni taasisi inayoishi ikiwa na umuhimu mkubwa kwa mashabiki na jamii, ilieleweka kwamba ni notisi ya muda mfupi, mchezo wa mwisho dhidi ya Middlesbrough ulichezwa pasipo mashabiki wa Chelsea.

“Lakini kwa notisi hii, FA hawana cha kujitetea, inabidi waruhusu kuuzwa kwa tiketi kwa mashabiki wa Chelsea ilimradi pesa zitakwenda kwa watu wa Ukraine”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe