Mchezaji ambaye anaichezea klabu ya Crystal Palace kwa mkopo akitokea Chelsea Conor Gallagher amekili kuvunjika moyo baada ya kutokuwepo kwenye mchezo wa nusu fainali ya FA Cup kwenye uwanja wa Wembley dhidi ya Chelsea.

Conor Gallagher ambaye anaitumikia klabu ya Palace kwa mkopo, ameshindwa kucheza mchezo wa nusu fainali ya FA Cup dhidi ya klabu yake mama siku ya jumapili, baada ya Chelsea kuwakatalia ombi lao la kutaka kumruhusu kucheza mchezo huo.

Conor Gallagher, Conor Gallagher: Nilitaka Kuwepo Uwanjani, Meridianbet

“Ilikuwa ngumu sana kuangalia. Ilibidi nikubali kwamba sikufanikiwa kucheza lakini niliangalia mchezo, nilikuwa nataka kuwepo uwanjani na kucheza.” Alinukuliwa Conor kwenye kikao na waandishi wa habari.

“Kucheza kwenye mchezo kama huu wa nusu faianali ya FA Cup kwenye uwanja wa Wembley ni ndoto ya kila mchezaji kwenye maisha yake ya soka, anataka kucheza mechi kama hizi.

“Lilikuwa tukio zuri kwa klabu kuwa kwenye uwanja wa Wembley na kucheza mchezo wa nusu fainali. Najivunua wao, ulikuwa mchezo mzuri wa kuangalia. Chelsea walicheza vizuri na alikuwa kwenye ubora wa juu siku ile.”

Conor Gallagher kwa sasa akili yake amewekeza kuweza kuisaidia klabu yake ya Palace,  kumaliza kwenye nafasi za juu kwenye ligi kuu ya Uingereza kwa mara ya pili kwenye historia ya klabu hiyo.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa