Hatimaye zile harakati za kuhakikisha wanawake wanakuwa kwenye nyanja mbalimbali duniani zimeanza kuonekana kwenye michezo, hii ni baada ya mwanamama Debbie Hewitt kutangazwa kuwa mwenyekiti wa chama cha soka cha Uingereza FA.
Debbie Hewitt atachukua nafasi hiyo ya uenyekiti wa FA mwakani mwezi Januari, huku akichukua nafasi itakayoachwa wazi na Greg Klarke, ambaye alijiuzuru mwaka jana mwezi Novemba kufuatia kauli chafu alizotoa!

Kamati ya viongozi mbalimbali wa chama hicho iliyokaa ili kupendekeza jina la atakayekuwa mwenyekiti wa chama hicho ilifanya kikao na kutoa tamko kuwa imekubaliana kutoa jina la Debbie Hewett kutokana na uzoefu wake kwenye Uongozi katika sekta nyingi.
Akionekana kufurahia nafasi hiyo, Debbie alidai kuwa anashukuru kupata cheo hicho ambacho kinalenga kuleta mabadiliko makubwa kwenye mpira wa Uingereza.
Debbie pia alieleza shauku yake ya kufanya kazi pamoja na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo afisa mtendaji mkuu Mark Bullingham na timu yake nzima. Debbie pia alionesha kufurahia fursa ya kuongoza kiti na atahakikisha kuwa analeta maendeleo ya soka Uingereza.
Chukua namba yako ya akaunti na kiasi cha pesa unachotaka kuweka, sogea kwenye duka lolote la Meridianbet lililo karibu nawe utasaidiwa kuweka pesa.
Wamama wana moto sana wa uongozi
Wamama tuko vizuri