Kocha mkuu wa Manchester City Pep Guardiola ametaka Graham Potter apewe muda zaidi kama kocha wa Chelsea, baada ya City kuichabanga The Blues kipigo kikali cha pili kwenye Kombe la FA.

 

Guardiola Ataka Potter Apewe Muda Zaidi

The Blues walipata kipigo cha pili katika muda wa siku nne dhidi ya mabingwa hao wa Ligi Kuu, kwa kufungwa mabao 4-0 kwenye Uwanja wa Etihad.

Potter aliwakashifu wakosoaji wake mapema mwezi huu, akisisitiza anahitaji muda na subira kutoka kwa mashabiki na mmiliki Todd Boehly ili kutekeleza maono yake.

Guardiola yuko katika makubaliano hayo, akiamini kuwa mazingira aliyokutana nayo katika kuiongoza Barcelona kutwaa mataji matatu katika msimu wake wa kwanza wa kuifundisha 2008-09 kuwa ya kipekee.

Guardiola Ataka Potter Apewe Muda Zaidi

Guardiola amesema; “Ningemwambia Todd Boehly, ilikuwa ni furaha kukutana naye, lakini mpe muda, najua matokeo ni muhimu katika vilabu vikubwa lakini ningesema mpe muda. Nadhani kipindi cha pili leo ndivyo alivyo na alichokifanya Brighton kilikuwa bora. Wasimamizi wote wanahitaji muda na alikuwa sahihi. Tunahitaji muda katika msimu wa kwanza.”

Guardiola anaongeza kuwa alikuwa na matokeo Barcelona katika msimu wa kwanza lakini walikuwa na Lionel Messi kwa hivyo msimu mmoja ulitosha. Lakini ndio, katika usimamizi wa soka. Kucheza dhidi ya Man City katika kiwango walichonacho kwenye Kombe la Carabao au Kombe la FA si rahisi. Si kwa Graham, Chelsea au timu yoyote.

Guardiola Ataka Potter Apewe Muda Zaidi

Mabao mawili ya Riyad Mahrez, pamoja na mabao ya Julian Alvarez na Phil Foden, yalisaidia kurahisisha kupita kwa City katika raundi ya nne, ambapo Arsenal au Oxford United wanasubiri.

Mchezaji wa Kimataifa wa Algeria Mahrez hasa alikuwa katika hali nzuri, na alifurahi kumruhusu mchezaji mwenzake Alvarez aliyeshinda Kombe la Dunia kupiga penalti ya mapema kabla ya kufunga mkwaju wake mwenyewe baadaye.

Aliiambia BBC Sport; “Ningechukua ya kwanza lakini Julian aliniuliza, hivyo nikasema bila shaka angeweza kuichukua yeye ni mshambuliaji, anapofunga ni vyema kwake. Nilitaka kuchukua la pili.”

Guardiola Ataka Potter Apewe Muda Zaidi

Kila msimu wanajaribu kuhusika katika kila mashindano, bado wako katika yote. Wanapaswa kuendelea, wanastahili kwa jinsi wanavyocheza.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa