Klabu ya Manchester City imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la shirikisho la soka nchini Uingereza Fa Cup baada ya kuwafunga majirani zao klabu ya Manchester United mabao mawili kwa moja leo katika dimba la Wembley.
Manchester City wamefanikiwa kutwaa ubingwa wao wa saba wa michuano ya kombe Fa Cup na kua miongoni mwa timu zilizotwaa michuano hiyo mara nyingi, Man City walifanikiwa kupata magoli yao ya ushindi kupitia kwa Ilkay Gundogan aliefunga mabao yote mawili huku bao la Man United likifungwa kwa mkwaju wa penati na Bruno Fernandes.Klabu ya Man City inaendelea kuweka matumaini hai katika ndoto zao za kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja yaani Treble baada ya kufanikiwa kushinda taji lake la pili msimu huu, Huku wakiwa wamebakiwa na fainali moja ya ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Inter Milan ili kutimiza mataji matatu.
Klabu ya Manchester United ilikua ina nafasi ya kuendelea kulinda rekodi yao ya kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja ambayo wanashikiliwa wao tu mpaka sasa, Lakini wameshindwa baada ya kukubali kipigo katika mchezo wa leo dhidi ya majirani zao klabu ya Manchester City.Klabu ya Manchester City baada ya kutwaa ubingwa hup leo macho yao watayaelekeza katika mchezo wao wa fainali ya ligi ya mabingwa ulaya dhidi ya Inter Milan mwezi Juni 6 pale Instanbul Uturuki, Kama Man City wakifanikiwa kutwaa taji la ligi ya mabingwa ulaya watavunja rekodi ya Man United waliyoiweka mwaka 1999 ya kutwaa mataji matatu ndani ya msimu mmoja.