Son Heung-min amefurahia kurejea kwake katika kiwango cha kufunga mabao baada ya kufunga mabao mawili katika ushindi wa Tottenham wa Kombe la FA kwenye Uwanja wa Preston North End.
Mabao mawili ya kipindi cha pili katika ushindi wa 3-0 hapo jana yalimaliza mwendo tasa kwa Son, ambaye alikuwa amefunga mara moja tu katika mechi 13 alizocheza.
Spurs walikuwa wametatizika wakati huo, wakiwa nyuma katika kusaka nafasi ya nne bora kwenye Ligi ya Primia na kuona uvumi ukiongezeka juu ya mustakabali wa Antonio Conte.
Safari ya Kombe la FA hadi Deepdale ilitoa mapumziko kutoka kwa shinikizo hilo, hata hivyo, na Son akafanikiwa kuongoza safu. Akiwa amerejea kati ya mabao, mchezaji huyo anahisi matokeo hayo yanaweza kutoa mwanya kabla ya mechi ya Jumapili ijayo ya ligi dhidi ya Manchester City.
Aliiambia BBC SPORT; “Nilihitaji mabao kwa ajili ya kujiamini kwangu. Ilikuwa muhimu sana, yalikuwa ya aina ya nafasi ninazopenda kupiga. Kipindi cha kwanza nilipata nafasi kadhaa, zililenga lango na kipa aliokoa vyema. Kipindi cha pili waliingia kwenye mfumo.”
Jambo muhimu zaidi ni kupata bao hilo. Pia aliongezea kuwa ilikuwa muhimu aweze kuisaidia timu na kuingia raundi inayofuata na ana furaha sana. Kuna maneno mengi kuhusu uchezaji wao na jinsi wanavyocheza. Wamezingatia, wanafanya kile wanachopaswa kufanya na wanajua kile wanachopaswa kuboresha.
“Tuna nafasi kubwa ya kuboresha, kwa hivyo mchezo huu unaweza kutuletea nguvu nzuri kwa wikendi ijayo.”
Mabao ya Son yalikuwa yake ya kwanza katika Kombe la FA tangu alipofunga mabao dhidi ya Southampton Februari 2020. Kwa hakika, kila moja ya mabao yake manne ya mwisho kwenye shindano hilo yamepatikana katika raundi ya nne.
Spurs, kwa upande wake, sasa wamefuzu zaidi ya raundi ya nne kwa msimu wa nne mfululizo, msimu wao mrefu zaidi katika Kombe la FA tangu 1979 hadi 1983, ingawa wametolewa katika raundi ya tano katika kampeni tatu zilizopita.
Harry Kane alibaki kwenye benchi siku ya jana na ilikuwa mara ya kwanza hajashiriki katika mechi ya Tottenham tangu Oktoba 2021, akihitimisha msururu wa mechi 68 mfululizo.