Mchezaji kiungo wa kati wa klabu ya soka ya Chelsea, Cesc Fabregas ana imani kwamba itakuwa ni vigumu sana kwa Wanabluu hao kuendelea kuwa na Eden Hazard mwenye umri wa miaka 27 klabuni hapo.

Mwezi wa saba mchezaji huyo ambaye ni raia wa Ubelgiji alitaka kuamsha Darajani pale ila klabu yake ikakataa kabisa kumpiga bei. Pia, kiungo mwenzake, Ross Barkley anasema kwamba kwa hivi sasa Hazard ni bora zaidi ya Lionel Messi wa Barcelona na Cristiano Ronaldo!

Fabregas anawindwa na Waitaliano

Klabu inayoshiriki Serie A, Italia, AC Milan imeonesha nia ya wazi wazi ya kumnasa Fabregas mwenye umri wa miaka 31 na kwa sasa wapo tayari kumnasa mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania ifikapo mwanzoni mwa mwaka ujao kwa mujibu wa Mundo Deportivo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa