“When you think all is lost, the future remains.”

Hii ni sentensi fupi sana anayoitumia Mzee wa Kaliua, Oscar Oscar katika maelezo yake kule WhatsApp. Wenye namba zake mnaweza kuwa mashahidi wa hilo.

farid
Oscar Oscar

Tafsiri yake isiyo rasmi ni kuwa, “unapoona umepoteza kila kitu leo, bado unabakiwa na kitu kimoja, hicho kitu ni kesho”. Kesho huwa hapotei mpaka itakapofika na kuitwa leo.

Katikati ya ukichaa wa mambo yake yote, sikutegemea kukutana na kauli ya busara kama ile kutoka kwa mvutaji kama Oscar Oscar. Nimemzoea kwa ukorofi na utukutu zaidi kuliko hekima.

Hata mara ya kwanza niliyokutana nae, alinieleza historia yake na misukosuko aliyokutana nayo. Si vema kueleza hapa ila kuna muda aliacha hadi kazi yake katika harakati za kuandaa kesho yake. Ndiyo maana anayapenda sana haya maneno.

WHEN YOU THINK ALL IS LOST THE FUTURE REMAINS.

Farid rudi usome tena hiyo sentensi halafu nikuambie kitu. Katika haya maisha zipo nyakati ngumu. Nyakati ambazo binadamu unahisi umepoteza kila kitu. Hizi ni nyakati ambazo wengi hukata tamaa.

Katika nyakati ambazo wengi hukata tamaa ndizo nyakati ambazo wengi hupoteza lengo na kupotea. Lakini ndizo nyakati ambazo wachache walio wavumilivu hudumu na kufanikiwa.

Basi Farid unaweza kuchagua kundi la kusimama kati ya hayo. Kundi la wanaokata tamaa na kupotea na kundi la wanaovumilia na kudumu.

farid, Farid Sikia Maneno ya Oscar Oscar, Meridianbet

Kama unafikiria kukata tamaa Farid kwasababu unahisi umepoteza kila kitu leo, kumbuka kuwa bado una kesho. Kesho bado haijapotea kabla haijafika. Lakini kesho tamu inaletwa na leo chungu.

Unaweza kuona kama ndoto zako hutazifikia. Unaweza kuona kama ulipo ndio mwisho wako lakini kumbuka unapohisi umepoteza kila kitu bado kesho yako ipo mikononi mwako. Ni wewe kuamua kuitengeneza.

Wewe piga kinanda chako. Usitazame yanasemwa nini juu yako. Kikubwa kwako kiwe, bado una siku inayoitwa kesho. Hiyo ndiyo muhimu zaidi Farid.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

kane, Kane Aweka Wazi Maazimio Yake Kucheza UEFA., MeridianbetBASHIRI SASA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa