Raisi wa Sampodoria, Massimo Ferrero ameweka wazi kuwa anaona msimu ndiyo umeisha! Ferrero ansema kuwa kuna haja ya kukubali kuwa msimu 2019/20 inadidi uishe hapa kwa sababu hakuna maana ya kuendelea kukimbizana uwanjani bila mashabiki.

Mashabiki kwenye soka huongeza radha ya soka na ushindani. Pia mashabiki huwa sehemu kubwa ya mapato ya vilabu pia. Kutokana na Changamoto ya Virusi vya Corona, mechi Ligi zote zimesimama na nyingine zikiwa katika maamuzi ya kufanywa kuwa msimu batili.

Lakini kutokana na hali na maendeleo ya mapambano dhidi ya virusi vya Corona, FIGC -Italia wamefanya kikao kujadili namna gani wanaweza kuendelea na mazoezi na hata kucheza mechi kabisa.

Baadhi ya klabu zinaona kuna haja ya kumalizia mechi zilizosalia za Ligi huku zingine zikiona kuna haja ya kuufuta msimu huu au kuumaliza. Sampodoria kupitia raisi wao, wanaungana na Brescia kukubaliana kuwa msimu uishie hapa.

Ferrero anasema inabidi waanze kufanya maandalizi mengine na kukubaliana kuwa msimu unaisha. Akisisitiza kuwa anaongea kutoka moyoni anasema kuwa angependa wamalizie sehemu iliyobaki, lakini kwa Sampodoria wangependelea zaidi wakiingia uwanja uwe umepambwa vyema na wapenzi wa timu, makelele na rangi kibao za unazi wa soka, anaamini hii ndio soka halisi. Mechi bila mashabiki haina maana.

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa