Mamlaka inayosimamia mchezo wa soka duniani, Fifa ipo na mpangi wa kubadilisha muda wa mashindano ya Kombe la Dunia.

Mashindano ya Kombe la Dunia yamekuwa yakifanyika kila baada ya miaka 4 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1930( kwa wanaume) na 1991 (kwa wanawake).

Mpango huu wa Fifa unatokana na pendekezo lililotolewa na Shirikisho la Soka nchini Saudi Arabia (SAFF). Katika pendekezo hilo, SAFF ilipendekeza muda wa mashindano ya Kombe la Dunia kuwa miaka miwili na sio 4 kama ilivyo. Vilevile, SAFF imegusia kufanyika kwa mabadiliko ya mfumo wa Fifa kwa kuzingatia ubora wa mchezo wa soka, usalama wa wachezaji sambamba na fursa za kibiashara.

SAFF wametoa pendekezo hilo wakiangazia namna ambavyo ulimwengu umeathiriwa na janga la Covid19 ikiwa ni sambamba na uwepo wa mashindano mengi ya timu za taifa ambayo yataleta tija bila kuathiri viwango vya wachezaji.

Pendekezo la SAFF liliwasilishwa kwenye mkutano mkuu wa Fifa na limepigiwa kura 166 za ndio ikiwa ni sambamba na kura 22 za hapana miongoni mwa mashirikisho ya soka kutoka nchi mbalimbali duniani.

Endapo Kombe la Dunia litafanyika kila baada ya miaka 2, baadhi ya mashindano ikiwepo mashindano ya Ulaya ambayo hufanyika kila baada ya miaka 4 (mara nyingi ni miaka ya katikati kabla ya kombe la dunia) itaathirika kwa kiasi kikubwa.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

River Plate, River Plate, Enzo Perez Aonesha Uwezo Golini., MeridianbetBASHIRI SASA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa