FIFA ilisitisha mashirikisho ya kitaifa ya mpira ya miguu ya Pakistani na Chad siku ya Jumatano kufuatia mizozo ya jinsi gani mashirikisho hayo yanapaswa kuendeshwa.

Shirikisho la soka la Pakistani linajulikana kama PPF, limesimamishwa baada ya kufanya kosa la “kuingilia kama mtu wa tatu” (third-party interference) kwa mara ya pili ndani ya miaka minne baada ya kundi la maafisa na waandamanaji kuzingira makao makuu ya shirikisho hilo mwezi uliopita.

Waandamanaji hao wanaopinga “Kamati ya kuhalisha” iliyoteuliwa na FIFA kuendesha michezo nchini humo baada ya mapigano ya muda mrefu na maafisa hao. Uvamizi wa makao makuu ya PPF, tayari umeharibu mashindano ya ubingwa ya kitaifa ya wanawake.

FIFA

“Kusimamishwa huku kutaondolewa FIFA endapo itapata uthibitisho kutoka kwa kamati ya kuhalalisha ya PFF kwamba majengo, akaunti, usimamizi na njia za mawasiliano za PPF ziko tena chini ya udhibiti kamili na inaweza kuendelea kutekeleza agizo lake bila kizuizi chochote,” ilisema FIFA.

Hapo awali Pakistani ilisimamishwa kutoka Oktoba 2017 hadi Machi 2018 baada ya FIFA kupinga uamuzi wa mahakama kumteua msimamizi wa nje kuendesha PFF baada ya mzozo mwingine juu ya uchaguzi uliopingwa. Aidha, Shirikisho la Mpira wa Miguu la Kimataifa FIFA linapinga mahakama au serikali kuhusika katika mizozo ya mpira wa miguu.

FIFA NA PPF

Kusimamishwa kwa Chad kunakuja baada ya serikali ya nchi hiyo ya Afrika kujaribu kuvunja shirikisho la kitaifa la soka na kuteua maafisa wapya kuendesha mchezo huo. FIFA itaondoa kusimamishwa huko ikiwa serikali itafuata maamuzi ya kumrudisha raisi wa shirikisho la soka la nchi hiyo.

Chad iliondolewa kwenye kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwezi uliopita wakati Shirikisho la Soka la Afrika liliagiza lipoteze michezo miwili kutokana na mzozo huo.


INAWEZEKANA KUWA MILIONEA BILA KUVUJA JASHO NA KASINO YA ODD ONE OUT.

Odd One Out kutoka Meridianbet ni moja ya kasino maridhawa yenye picha halisi, ambayo inakupa nafasi ya kushinda kadri uwezavyo na kuwa milionea mara baada ya mzunguko kukamilika.

FIFA, FIFA Yaisimamisha Pakistani na Chad, Meridianbet

CHEZA HAPA

4 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa