Kikosi cha timu ya taifa ya Afrika Kusini, Bafana Bafana, kimeondoka kuelekea Mexico kushiriki Fainali za Kombe la Dunia 2026 baada ya kukamilisha maandalizi ya mwisho ya safari hiyo muhimu kwa soka la taifa hilo.
Safari ya kikosi hicho ilikuwa imepangwa kufanyika Jumapili, lakini ilikumbwa na kuchelewa kufuatia changamoto za upatikanaji wa viza kwa baadhi ya wachezaji na maafisa wa timu. Hali hiyo ilisababisha ratiba ya kuondoka kusogezwa mbele kwa muda mfupi.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
“Changamoto za viza kwa baadhi ya wachezaji zilisababisha safari ya Bafana Bafana kuchelewa, lakini taratibu zote zimekamilika na kikosi sasa kiko njiani kuelekea Mexico,” zimeeleza taarifa kutoka kambi ya timu hiyo.
Wawakilishi hao wa Afrika wanatarajia kuandika historia kwa kushiriki mechi ya ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026, ambapo watakutana na wenyeji Mexico katika mchezo utakaopigwa Juni 11, 2026 mbele ya maelfu ya mashabiki.
“Bafana Bafana wako tayari kwa changamoto ya Kombe la Dunia na sasa macho yote yanaelekezwa kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya Mexico,” imeongeza taarifa hiyo huku mashabiki wa Afrika Kusini wakisubiri kwa hamu kuona timu yao ikianza kampeni ya michuano hiyo mikubwa duniani.


