Kocha wa timu ya taifa ya Hispania, Luis de la Fuente amesema bado hajamfuta beki wa kulia Dani Carvajal katika kikosi cha Kombe la Dunia, lakini nyota huyo atalazimika kuthibitisha kiwango chake cha utimamu wa mwili kabla ya mashindano hayo kuanza.
Carvajal alipata majeraha ya mguu wa kulia wakati wa mazoezi ya klabu yake Real Madrid wiki iliyopita, hali iliyozua mashaka kuhusu nafasi yake katika kikosi cha Hispania kitakachoshiriki Kombe la Dunia litakalofanyika Marekani, Canada na Mexico kuanzia Juni 11 hadi Julai 19.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Akizungumza na waandishi wa habari Jumatano, De la Fuente alisema kuwa mchezaji huyo bado ana nafasi ya kurejea ikiwa ataonyesha maendeleo mazuri katika mechi zilizobaki za msimu huu.
“Carvajal ni mtu muhimu sana ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo. Nilizungumza naye jana hivyo ninafahamu kinachoendelea,” alisema De la Fuente.
Kocha huyo alieleza kuwa Carvajal hana jeraha kubwa sana, lakini anahitaji muda zaidi ili kurejea katika kiwango chake cha kawaida kabla ya kuitumikia Hispania katika michuano hiyo mikubwa duniani.
“Hana tatizo kubwa maalum, lakini anahitaji muda ili kurudi kwenye kiwango chake bora. Tutaangalia katika mechi zilizobaki kama atapata nafasi ya kucheza na kuonyesha kiwango kinachohitajika,” aliongeza kocha huyo.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 34 amecheza mechi moja pekee kwa Hispania mwaka 2025, huku akipata ushindani mkubwa ndani ya kikosi cha Real Madrid kutoka kwa beki wa England Trent Alexander-Arnold. Hispania itaanza kampeni yake ya Kombe la Dunia dhidi ya Cape Verde Juni 15 kabla ya kukutana na Saudi Arabia na Uruguay katika kundi H.


