Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limetangaza kuanzisha uchunguzi kuhusu vurugu zilizozuka baada ya mchezo wa fainali ya michuano ya Dunia, ambapo Hispania iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Argentina baada ya muda wa nyongeza na kutwaa taji lake la pili la dunia.
Mvutano uliongezeka mara baada ya Ferran Torres kuifungia Hispania bao la ushindi katika muda wa nyongeza. Kabla ya hapo, Argentina ilikuwa tayari imebaki na wachezaji 10 kufuatia Enzo Fernández kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 93 ya muda wa kawaida baada ya kupata kadi ya pili ya njano.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Baada ya filimbi ya mwisho, kiungo wa Argentina Leandro Paredes alihusika katika mabishano na wachezaji wa Hispania, akiwemo Eric García na Gavi, hali iliyosababisha wachezaji wa pande zote mbili kuanza kusukumana na kuzua vurugu uwanjani. Kocha wa Argentina, Lionel Scaloni, alionekana akijaribu kutuliza hali huku maafisa wa mechi wakisaidia kuwatenganisha wachezaji.
“FIFA imemteua mwendesha mashtaka wa kamati za nidhamu na maadili ili kuchunguza matukio yote yaliyotokea baada ya mchezo na kubaini hatua zinazofaa kuchukuliwa,” ilieleza taarifa ya shirikisho hilo.
Hadi sasa, FIFA haijaweka wazi ni lini uchunguzi huo utakamilika au iwapo kutakuwa na adhabu dhidi ya wachezaji au maafisa waliohusika. Hata hivyo, matokeo ya uchunguzi huo yanatarajiwa kubainisha hatua za kinidhamu zitakazochukuliwa kufuatia vurugu zilizotia doa fainali hiyo ya mashindano ya Dunia.


