FIFA Yaishutumu UEFA Kwa “Kampeni ya Kuchafua Jina” Dhidi ya Infantino

Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) limeishutumu Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA) kwa kuendesha kile ilichokiita kuwa ni “kampeni ya kuchafua jina” dhidi ya taasisi hiyo pamoja na Rais wake, Gianni Infantino.

FIFA Yaishutumu UEFA Kwa “Kampeni ya Kuchafua Jina” Dhidi ya InfantinoMvutano huo unatokana na mpango wa FIFA Forward Enterprise (FFE) uliositishwa mwishoni mwa Julai 2026. Mpango huo ulilenga kuhamisha sehemu ya haki za kibiashara zinazohusiana na mashindano ya FIFA, ikiwemo Kombe la Dunia, kwa wawekezaji binafsi, lakini ulikumbana na upinzani mkubwa kutoka UEFA na mashirikisho mengine ya soka.

UEFA imekuwa ikitafuta nyaraka na ushahidi kupitia mahakama za Marekani kwa ajili ya uwezekano wa kuchukua hatua za kisheria nchini Uswisi dhidi ya Infantino na baadhi ya maafisa wa FIFA. FIFA, kwa upande wake, imeziomba mahakama kuchelewesha au kukataa maombi hayo.

FIFA Yaishutumu UEFA Kwa “Kampeni ya Kuchafua Jina” Dhidi ya InfantinoKatika nyaraka zilizowasilishwa mahakamani, FIFA imedai kuwa hatua zinazochukuliwa na UEFA kwa kutumia taratibu za kisheria ni sehemu ya juhudi za kuharibu hadhi ya FIFA na uongozi wake. FIFA pia imehoji sababu ya UEFA kutafuta ushahidi huo wakati hakuna kesi rasmi ya jinai iliyofunguliwa nchini Uswisi.

FIFA Yaishutumu UEFA Kwa “Kampeni ya Kuchafua Jina” Dhidi ya InfantinoMgogoro huo umeongeza presha kwa Infantino kuelekea uchaguzi wa urais wa FIFA unaotarajiwa kufanyika mwaka 2027, huku tofauti za kimtazamo na kiutawala kati ya FIFA na UEFA zikiendelea kuchochea mvutano ndani ya uongozi wa soka duniani.

Acha ujumbe

Meridianbet

Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.