Gyokeres Aibuka Shujaa Sweden Ikifuzu Kombe la Dunia

Mshambuliaji Viktor Gyökeres ameibuka shujaa wa Sweden baada ya kufunga bao la dakika za mwisho lililoihakikishia ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Poland na kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Amerika Kaskazini.

Gyokeres Aibuka Shujaa Sweden Ikifuzu Kombe la DuniaMchezo huo uliochezwa katika dimba la Strawberry Arena, Solna, ulikuwa na ushindani mkubwa huku Sweden wakitangulia kufunga dakika ya 20 kupitia Anthony Elanga aliyemalizia pasi safi kwa shuti kali lililogonga mwamba na kuingia wavuni.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa 

Poland hawakukata tamaa na walirejea mchezoni dakika ya 33 kupitia Nicola Zalewski aliyefunga bao la kusawazisha, kabla ya Sweden kurejesha uongozi tena kupitia Gustaf Lagerbielke aliyefunga kwa kichwa kufuatia mpira wa adhabu.

Gyokeres Aibuka Shujaa Sweden Ikifuzu Kombe la DuniaKipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Poland walifanikiwa kusawazisha tena kupitia Karol Świderski aliyemalizia pasi ya karibu, na kufanya mchezo kuwa mgumu kwa pande zote huku kila timu ikisaka ushindi.

Dakika ya 88 ndipo Sweden walipopata bao la ushindi kupitia Gyökeres aliyewahi mpira uliorudi baada ya kugonga mwamba, na kuutumbukiza wavuni kwa ustadi mkubwa. “Huu ni ushindi wa moyo na mapambano hadi mwisho,” ilielezwa baada ya mchezo huo uliojaa presha kubwa.

Gyokeres Aibuka Shujaa Sweden Ikifuzu Kombe la DuniaKwa ushindi huo, Sweden wanarejea katika fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2018, huku Poland wakikosa nafasi hiyo licha ya kupambana kwa nguvu, na hivyo kumaliza ndoto yao ya kushiriki michuano hiyo mwaka huu.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.