Rais wa Real Madrid Florentino Perez ameripotiwa kuanza kuandaa orodha fupi ya makocha watakaorithi mikoba ya Carlo Ancelotti, licha ya kiwango kizuri cha klabu hiyo kwa sasa.

Tangu arejee Bernabeu majira ya kiangazi yaliyopita, Ancelotti hajaleta mafanikio yoyote alipoiongoza Madrid kutwaa LaLiga na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita.
Lakini, licha ya kuanza kwa nguvu mwaka huu, Perez tayari ameanza kutafuta mrithi wa kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 na anatarajia kupata chaguo sawa na kocha wa zamani Zinedine Zidane, huku magwiji wawili wa klabu hiyo wakipigiwa debe.
Kulingana na Media Foot, Perez anataka mchezaji wa zamani kama Zidane, kuchukua jukumu na ameweka macho yake kwa Raul na Xabi Alonso.

Raul, ambaye aliichezea Madrid zaidi ya mechi 500 katika maisha yake ya mpira, kwa sasa anaiongoza timu ya Castilla, tangu kuteuliwa kwake mwaka 2019. Wakati huo huo, Alonso amepatikana hivi majuzi tangu alipoacha nafasi yake kama kocha wa Real Sociedad B mwezi Mei.
Alonso pia anapendekezwa kurithi mikoba ya Gerardo Seoane kama kocha wa Bayer Leverkusen, baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kuanza vibaya msimu wa 2022-23. Chombo hicho hicho kinapendekeza Perez pia anafuatilia hali ya bosi wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann, ikiwa atapatikana katika siku zijazo.