Mshauri wa Infantino FIFA, Carlos Cordeiro Ajiuzulu Kupinga Mpango wa FFE

Mshauri Mkuu wa Rais wa FIFA, Carlos Cordeiro, amejiuzulu nafasi yake mara moja baada ya kupinga vikali mpango wa kuanzishwa kwa kampuni ya uwekezaji ya FIFA Forward Enterprise (FFE), ambao unatajwa kulenga kuuza sehemu ndogo ya umiliki wa mapato ya michuano ya Dunia kwa wawekezaji binafsi. Uamuzi huo unakuja wakati Rais wa FIFA, Gianni Infantino, akiendelea kutetea mpango huo licha ya kuibua mjadala mkubwa ndani ya familia ya soka duniani.

Mshauri wa Infantino FIFA, Carlos Cordeiro Ajiuzulu Kupinga Mpango wa FFECordeiro amesema hakuhusika katika kuandaa pendekezo hilo na hawezi kuunga mkono hatua ambayo anaamini itadhoofisha mustakabali wa mchezo wa soka. Amesema FIFA tayari ina uwezo mkubwa wa kifedha, ikiwa na akiba ya mabilioni ya dola na bila madeni, hivyo hakuna ulazima wa kuuza sehemu ya mali yake yenye thamani kubwa zaidi ili kupata fedha za maendeleo.

mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu

“Naweka wazi kuwa sikushiriki katika pendekezo hili na ninalipinga kabisa. Ni mpango mbaya kwa vyama wanachama wa FIFA, ni mbaya kwa mchezo wa soka na ni kuhatarisha mustakabali wa mchezo kwa manufaa ya muda mfupi,” amesema Cordeiro, akisisitiza kuwa kuuza sehemu ya haki za taji la Dunia ni sawa na kuweka rehani mustakabali wa soka bila sababu za msingi.

Mshauri wa Infantino FIFA, Carlos Cordeiro Ajiuzulu Kupinga Mpango wa FFEAmeongeza kuwa baada ya kutafakari kwa kina, ameona hawezi kuendelea na nafasi yake kama mshauri wa rais wa FIFA kwa kuwa wajibu wa shirikisho hilo ni kulinda mchezo wa soka kwa vizazi vijavyo badala ya kutanguliza maslahi ya kibiashara. “Pale ambapo maslahi ya biashara yanagongana na maslahi ya soka, soka lazima lipewe kipaumbele,” amesema.

Mshauri wa Infantino FIFA, Carlos Cordeiro Ajiuzulu Kupinga Mpango wa FFEWakati huo huo, mashirikisho ya soka ya Ulaya (UEFA), Amerika Kaskazini na Kati (CONCACAF) pamoja na Asia (AFC) yameonyesha upinzani wao dhidi ya mpango huo, huku UEFA ikitangaza kuwa vyama vyake vyote 55 vinaweza kususia mashindano ya FIFA endapo pendekezo hilo litaendelea. FIFA, kwa upande wake, imekanusha madai kuwa inalenga “kuuza” michuano ya Dunia na kusema mchakato wa mashauriano bado unaendelea.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.