Nyota wa klabu ya Manchester United Cristiano Ronaldo amefunga goli lake la 806 kwenye dimba la Old Trafford siku ya Jumamosi na kuweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa FIFA.
Usiku wa jumamosi Ronaldo alifunga hat-trick yake ya pili kwenye ligi kuu ya Uingereza huku ikiwa ni hat-trick ya 59 kwenye maisha yake ya soka, kwenye ushindi wa 3-2 United alioupata dhidi ya Tottenham umewarudisha kwenye nafasi ya nne wakiwa ponti mbili zidi ya Arsenal mwenye michezo 4 mkononi.
Magoli 806 ambayo Cristiano Ronaldo amefanikiwa kufunga na kupita rekodi iliyowekwa na Josef Bican mwenye magoli 805, alifunga magoli 5 akiwa na Sporting Lisbon, 136 Man Utd, 450 Real Madrid, 101 Juventus na 115 akiwa na timu ya taifa ureno.
“Hakuna kitu kinachoweza kuishinda furaha ya kurudi uwanjani na kuisaidia timu kushinda na juhudi,” aliandika Ronaldo kwenye ukurasa wake wa Instagram baada ya mchezo kuisha.
“Tumethibitisha kuwa tunaweza kuifunga timu yeyote na siku yeyote ilimradi tu tunafanya kazi kwa kujituma na kuwa wamoja.”
Huku klabu ya Man Utd wao wakichapisha kwenye mtandao wa Twitter baada ya mchezo kuisha “Superhuman.”
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.