Taifa Stars Yaelekea Rwanda kwa FIFA Series 2026, Msuva Akosekana

Kikosi cha Tanzania Taifa stars kimeanza safari kuelekea nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki michuano ya FIFA Series 2026 inayotarajiwa kuanza hivi karibuni, huku kikosi hicho kikiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mashindano hayo ya kimataifa.

Taifa Stars Yaelekea Rwanda kwa FIFA Series 2026, Msuva Akosekana  Safari hiyo inafanyika chini ya Kocha Mkuu Miguel Gamondi ambaye amepewa rasmi jukumu la kuinoa timu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili, akipewa dhamana ya kujenga kikosi imara kitakachoweza kushindana katika mashindano mbalimbali yajayo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Katika mabadiliko ya kikosi, kiungo Morice Abraham ameongezwa kwenye msafara wa Taifa Stars kuchukua nafasi ya winga Simon Msuva ambaye ameshindwa kujiunga na timu hiyo kutokana na changamoto za usafiri.

Taifa Stars Yaelekea Rwanda kwa FIFA Series 2026, Msuva Akosekana  
Akizungumzia hali hiyo, Gamondi alisema “Tulifanya kila liwezekanalo kuhakikisha Msuva yupo kwenye kikosi, lakini haikuwezekana kutokana na hali ilivyo sasa. Tumemjumuisha Morice Abraham ili kuimarisha timu.”

Kwa mujibu wa taarifa, Msuva anayekipiga soka nchini Iraq ameshindwa kusafiri kutokana na kukosekana kwa safari za ndege kufuatia mvutano wa kijeshi unaoendelea kati ya Iran na Marekani.

Taifa Stars Yaelekea Rwanda kwa FIFA Series 2026, Msuva Akosekana  Pamoja na changamoto hiyo, benchi la ufundi linaamini kuwa wachezaji waliopo wataweza kujaza pengo hilo na kuendelea kupambana kwa ajili ya kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mashindano hayo.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.