Rais wa FIFA, Gianni Infantino, ameendelea kukumbana na shinikizo kuelekea uchaguzi wa urais wa shirikisho hilo wa mwaka 2027 baada ya Shirikisho la Soka la Wales (FAW) kutangaza kuondoa rasmi uungwaji mkono wake, huku Shirikisho la Soka la England (FA) likitarajiwa kufuata hatua hiyo.
Hatua hiyo imechochewa na kushindwa kwa mpango wa FIFA wa kuuza sehemu ya hisa katika taasisi mpya inayosimamia mashindano makubwa, ikiwemo michuano ya Dunia, kwa wawekezaji binafsi. Mpango huo, uliolenga kukusanya hadi dola bilioni 4.2, ulisitishwa baada ya kupingwa vikali na wadau mbalimbali wa mchezo huo.
mpira wa miguu, kubeti mpira wa miguu, bashiri soka, soka, beti kwenye soka, odds za soka, bashiri mpira wa miguu, beti za soka, beti mechi za soka, odds za kubeti mpira wa miguu
FAW ilieleza kuwa imefikia uamuzi huo baada ya kupoteza imani na namna Infantino anavyoendesha FIFA, ikidai kumekuwa na mapungufu makubwa katika uongozi na maamuzi yanayohusu mustakabali wa soka duniani.
“Tumeamua kuondoa uungwaji mkono wetu kwa Bw. Gianni Infantino kutokana na kushuka kwa viwango vya utawala bora, uongozi, maadili, usimamizi wa wadau na maamuzi yanayohusu maslahi ya mchezo. Kushindwa kuweka maslahi ya soka mbele ni jambo ambalo hatuwezi kulikubali,” ilisema FAW kupitia taarifa yake.
Mbali na Wales, mashirikisho ya soka ya Ulaya (UEFA) na Amerika Kaskazini, Kati na Karibiani (CONCACAF) nayo yameonyesha kutoridhishwa na uongozi wa Infantino. Hali hiyo inaweka sintofahamu kuhusu nafasi yake ya kutetea urais kwa muhula wa 2027 hadi 2031, licha ya kuwa aliwahi kuchaguliwa bila kupingwa katika chaguzi mbili zilizopita tangu alipochukua nafasi ya Sepp Blatter mwaka 2016.


