AFCON: Referee Amaliza Mchezo Kabla ya Muda

AFCON, kwenye mchezo kati ya Tunisia na Mali referee amemaliza mpira sekunde kumi kabla ya dakika tisini kufika na kusababisha kuleta sintofahamu kwa wachezaji na Tunisia ambao walikuwa nyuma kwa goli moja.

Mali walikuwa wanaongoza kwa 1-0 baada ya Ibrahima Koné kufunga kwa mkwaju wa penati, kabla ya Tunisia kukataliwa kipindi cha pili baada ya mchezaji wa zamani wa Sunderland Wahbi Khazri mkwaju wake kuokolewa na  Ibrahim Mounkoro.

AFCON
AFCON

Kipindi cha pili kilitumia muda mwingi kusimamisha mchezo kutokana na maamuzi dhidi ya penati mbili, pia kulikuwa na muda wa kunywa maji, kusubiri maamuzi ya VAR na majeruhi yalichangia kusimamisha mchezo.

Kabla ya refarii kupuliza kipenga cha kumaliza dakika ya 89 ya mchezo, awali referee alitaka kumaliza mpira dakika ya 85, baada ya hasira za wachezaji kuanza kumzonga na kutumia muda kadhaa kabla mpira kuandelea baadae.

AFCON
AFCON

Kutokana na mchezo kutumia muda mwingi kusimama ilitegemewa kuwa referee angeongeza muda mwingi, lakini aliwashangaza baada kupunguza muda wa kumaliza mchezo tofauti na ilivyotarajiwa, baada ya kupuliza kipenga cha kumaliza dakika 89 na sekunde 44.

Mambo yalikuwa mazuri kwa Mali ambao walikuwa wanashangilia, huku upande wa Tunisia wakiwa wanamzonga referee kwenye dimba la Limbe wakitaka kujua kwa nini kamaliza mpira kabla ya muda, huku referee alisimamia msimamo wake kuwa muda umekwisha na kuomba msaada wa ulinzi kuweza kuzuia hatari kwa refa.


JIACHIE NA ALMIGHTY AZTEC

Ni muda wako kujiachia na mchezo maridhawa wa Almighty Aztec katika kasino bomba za meridianbettz. Nafasi ya kutengeneza mkwanja iko mikononi mwako kazi ni kwako.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe