BAADA ya kuhusishwa na uhamisho wa Simba, beki wa Biashara United ya Mara, Abdulmajid Mangalo amefunguka kukataa ofa hiyo huku akitarajia kujiunga na klabu nyingine.
Licha ya Biashara United kushuka daraja lakini beki huyo alionyesha kiwango bora kiasi cha kuzishawishi baadhi ya klabu za ligi kuu kuhitaji huduma yake kwa msimu ujao.