Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester City Vincent Kompany amekubali kuachia ngazi ya kuionoa klabu ya Anderlecht na kurudi uingereza ili kuinoa klabu ya Burnley.
Vincent Kompany alipendekezwa na mwenyekiti wa klabu hiyo Alan Pace kipindi ambacho alikuwa anapendekeza makocha ambao wanaweza kubeba mikoba ya Sean Dyche, ambaye alifungashiwa virago kwenye kipindi cha pasaka.
Mchezaji huyo wa zamani wa Man City amekuwa akiinoa klabu ya nchini kwake Ubelgiji Anderlecht tangu mwaka 2019, ni moja aina ya majina makubwa ambayo yalichaguliwa na Pace kutaka kuinua klabu hiyo.
Vincent Kompany mwenye miaka 36 atakuwa na kazi ya kufanya kuweza kuirudisha klabu hiyo ligi kuu ya Uingereza baada ya msimu kushuka daraja siku ya jumapili ikiwa chini ya kocha wa muda Mike Jackson ambaye ndiye alikuwa kwenye benchi katika mchezo wa mwisho.
Mpaka sasa bado hakuna taarifa kamili ikiwa Kompany ameshasaini mkataba na Clarets huku taarifa zikivuja kuwa tayari washafanya makubaliano ya awali limebaki la swala la Kompany kuweza kusaini mkataba na kuanza kazi.
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.