BAADA ya kurejea Yanga akitokea Simba, kiungo mshambuliaji, Bernard Morrison amevunja ukimya na kuahidi furaha tena kwa mashabiki wa klabu hiyo.
Morrison amefunguka kuwa “Nilikuwa hapa nikaondoka na sasa nimerejea tena, katika wakati huu naahidi kufanya kitu kikubwa zaidi kwa timu hii na mtaendelea kunipenda.”

“Nilisababisha maumivu na aibu kwa muda uliopita lakini bado mmenikubali kijana wenu kwani wote tunajua kuwa nyumbani ni nyumbani.”
“Kijana wenu nimerudi na nitafanya kila niwezalo kuwafurahisha kokote na muda wowote, tufanye kazi wote na kufanya klabu hii kubwa kuwa katika ubora wake.”