Golikipa wa zamani timu ya taifa ya Italia Gianluigi Buffon amesaini mkataba mpya na timu yake ya Parma ambayo inashiriki ligi ya Serie B wa mwaka mmoja ambao utamuweka kwenye klabu hiyo mpaka mwaka 2024.

Gianluigi Buffon alijiunga na klabu ya Parma akitokea klabu ya Juventus majira ya kiangazi baada ya kutumia miaka 20 nje ya klabu hiyo ambayo alianzia maisha yake ya uchezaji wa mpira wa kulipwa.

Gianluigi Buffon

Gianluigi Buffon ameshinda makombe 27 kwenye maisha yake ya soka, ikiwemo kombe la Dunia mwaka 2006 akiwa na timu ya taifa ya Italia na UEFA Cup mwaka 1999 akiwa na Parma.

Parma ilikuwa moja ya timu kubwa nchini Italia kwenye miaka 1990 hadi 2000 wakati ikiwa chini ya umiliki wa kampuni ya Parmalat, na walifanikiwa kushinda makombe makubwa matatu barani ulaya, mwaka 2003 baada ya kupata kashfa utatakatishaji fedha ilipelekea klabu hiyo kufirisika na kushuswa hadi Serie D.

Gianluigi Buffon hajafanikiwa tena kuchukua ubingwa wa UEFA tokea aachane na Parma, huku akifanikiwa kucheza fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya mara tatu akiwa na Juventus  2003, 2015 na 2017, pia amewai chezea klabu ya PSG kati ya mwaka 2018-2019 na kufanikiwa kuchukua ubingwa wa Ligue 1.


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa