UEFA wamepanga kuanza kutumia Video Assistant Referee (VAR) kwenye michezo ya nusu fainali ya Europa Conference League kulingana na taarifa zilizoropiwa nchini Italia.
Leicester City kwa mara ya kwanza wanacheza nusu fainali ya mashindano ya ulaya ambayo yanaandaliwa na UEFA baada ya kuiondoa klabu ya kutoka nchini Uholanzi PSV Eindhoven. Asante kwa magoli yaliofungwa na m James Maddison na Ricardo Pereira na kufanya mchezo kuisha kwa uwiano wa 2-1.

Kikosi cha Brendan Rodgers kinatarajiwa kuwa karibisha kikosi cha Jose Mourinho kwenye mchezo wa kwanza wa nusu fainali ambao utapigwa kwenye dimba la King Power Stadium April 28. Leicester watasafiri baada ya wiki kwenda Roma kwa ajiri ya mchezo wa nusu fainali ya pili.
Ukiondoa mashindano mengine ya UEFA ambayo VAR inatumika, ila mpaka sasa Europa Conference League, haikuwa kwenye mfumo wa VAR na awali ilipangwa kuanzishwa kwa mara kwanza kwenye mchezo wa fainali ambao utachezwa nchini Albania jijini Tirana May 25.
Kulingana na taarifa iliyoripotiwa na Corriere dello Sport, mfumo wa VAR utaanza kutumika kwenye nusu fainali zote mbili. Hii inamaana kuwa michezo yote ya nyumbani na ugenini ya City vs Roma na kati ya Marseille vs Feyenoord.
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.