Watu wengi hudhani mchezo wa gofu pekee ndio mchezo wa watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi. La hasha! Lewis Hamilton anakwambia “Formula 1 ni klabu ya wanaume matajiri”

Hamilton amezungumza hilo akijichukulia mfano yeye mwenyewe. Mpaka kufikia kuwa bingwa mara 7 wa F1, umewahi kujiuliza historia yake ipoje? Alifikaje kwenye F1 kwa mara ya kwanza?

Mchongo upo hivi, wakati Lewis Hamilton akiwa mtoto ambaye ametoka kwenye familia ya wafanyakazi wa kawaida sana ambapo pia alikulia kule Stevenage, baba yake (Anthony) alifanya vibarua mbalimbali ili kumuwezesha kijana wake kusoma.

Siku zilikwenda na bahati ikamuangukia Hamilton. Naam, McLaren na Mercedes walihusika sana katika kumuendeleza Hamilton kimasomo na akiwa na miaka 13 akaanza kuingia kwenye ramani za F1.

“Kukulia kwenye mazingira ya kawaida ya wafanyakazi, nisingeweza kufika hapa. Watu unaoshindana nao wanauwezo mkubwa wa kifedha. Tunapaswa kulifanyia hili kazi ili watu wengi waweze kushiriki, kwa matajiri na kwa watu wenye uwezo wa kawaida.” alisema Hamilton.

Formula 1, Formula 1 ni Klabu ya Matajiri, Lewis Hamilton., Meridianbet
Mich (kushoto) na baba yake Michael Schumacher (kulia)

Anachokisema Hamilton kina uhalisia ndani yake, Lance Stroll, Nicholas Latifi, Nikita Mazepin ambao wote wamejiunga na Formula 1 kwa siku za karibuni, ni watoto wa matajiri.

Mpinzani wake mkali msimu huu, Max Verstappen na Mich Schumacher wote ni watoto wa matajiri ambao pia baba zao waliwahi kuwa madereva wa Formula 1.

Hamilton akishirikiana na timu yake ya Mercedes, wamekuja na mpango wa kutaka kuwavutia watu wa jamii zote kuingia kwenye mchezo wa langalanga. Pamoja na hayo, wameweka mchakato wa kutaka kujua ni kwanini watu wa tabaka la chini hawaonekani kwenye mchezo huo.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

River Plate, River Plate, Enzo Perez Aonesha Uwezo Golini., MeridianbetBASHIRI SASA

ONI MOJA

  1. Mchezo unaonekana wa matajiri kwasababu ya vifaa vya mazoezi ni aghali sana ambapo si rahisi kwa mtu wa kawaida kumudu

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa