F1: Ratiba ya 2020 Imekamilika Rasmi!

Mchezo wa mbio za magari – Formula 1 [F1] ni kati ya michezo iliyoathiriwa na mlipuko wa Corona. Baada ya kurudi kwa michezo kadhaa, sasa ni rasmi ratiba ya 2020 imekamilika.

Mbio zilizokuwa zimepangwa kutimua vumbi katika nchi mbalimbali sasa ni rasmi kazi imeanza. Bahrain watakuwa wenyeji wa mbio mbili wakati Uturuki (Turkey) wakirejea kwenye ulimwengu wa Formula 1 kwa mara nyingine baada ya miaka 9 (tangu 2011).

Barhrain na Turkey wenyeji wa F1.

Wakati Abu Dhabi wakijiandaa kuwa wenyeji wa mchezo wa fainali Disemba 13, watahitimisha jumla ya mbio 17 zilizopangwa kuchezwa kwa mwaka 2020. Mpaka sasa, mbio 6 zimeshafanyika bila ya mashabiki. Kuelekea michezo 11 iliyosalia, mashabiki wataruhusiwa kwenye baadhi ya mbio hizi.

Ratiba ya mbio 11 za kukamilisha msimu wa F1, 2020

Istanbul Park ambayo mwanzoni haikuwa kwenye orodha ya viwanja vitakavyotumika mwaka huu, sasa itapelekea kuwa na viwanja vitano vitakavyo tumika mwaka huu kunako mbio za Formula 1. Mugello (Italia) , Nurburging (Ujerumani), Portimao(Ureno) na Imola (Italia) ni viwanja vinavyokamilisha idadi hiyo.

Kwa mwaka huu, Bahrain itakuwa ni sehemu ya kwanza kuwa wenyeji wa mbio hizi kwa mara mbili mfululizo baada ya Austria na Silverstone.

“Huu mwaka umetupatia changamoto kubwa na tunatoa shukrani kwa kila mtu kuanzia F1, FIA, timu shiriki na wadau wetu wote waliofanikisha jambo hili.

“Wakati tukiwa tunahuzunika kwa kushindwa kufanikisha baadhi ya mbio kwa mwaka huu kama zilivyokuwa zimepangwa, tunajiamini msimu huu umeanza vizuri na tutaendelea kufurahia utamaduni wetu pamoja na kuanzisha mbio mpya zitakazo waburudisha mashabiki wetu.” amesema raisi wa F1 – Chase Carey.


Beti Mbio za Mbwa Mubashara

Hii ni rahisi zaidi! Hapa USHINDI unaupata kwa kuchagua mbwa anayeshinda mbio na machaguo mengine yenye odds tamu.

Cheza Hapa

22 Komentara

    Hii ni habari nzuri kwa mashabiki wa mchezo huu

    Jibu

    Ratiba imekaa poa sana

    Jibu

    Ratiba imetulia

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Ninamatumain sana msimu huu wa formula 1 makampun mengi yatashiriki maana ni mchezo ambao tumeusubir kwa hamu kubwa kuona mashindano ya uendeshaji wa magar nq ratiba imekaa poa sana 👍

    Jibu

    Nic wapenz wambio hiz za magar walizmis

    Jibu

    Afadhali

    Jibu

    Iko Poa sana

    Jibu

    Imetulia kwa hamilton kukimbiza tena

    Jibu

    Nice update

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Nice

    Jibu

    Ratiba ipo bomba sana

    Jibu

    Good

    Jibu

    safii sana meridian

    Jibu

    ratiba sasa imekamilika

    Jibu

    Ratiba iko fresh

    Jibu

    Asante kwa ratiba nzuri

    Jibu

    Iko guda.

    Jibu

    mambo mazuri yaja
    tunasubilia kuona kwa hamu zote

    Jibu

    Mdogo Mdogo tutafika tu

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.