Baada ya kuwa na majadiliano ya hapa na pale, hatimaye timu zote 10 zinazoshiriki Mashindano ya Formula One [F1] zimesaini mkataba wa ‘Concord Agreement’.
Mkataba [Concord Agreement] uliopo kwa sasa unajumuisha timu zote, shirikisho pamoja na wamiliki wa F1. Mkataba wa Liberty Media unaisha mwishoni mwa mwaka huu na viongozi wa Formula One wamekuwa kwenye majadiliano na timu zinazoshiriki michuano hiyo kwa muda sasa, lengo likiwa ni kujiandaa na mkataba mpya utakaotumika kuanzia mwaka 2021-2025 ikiwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa kwenye Formula One.
Timu ya Ferrari, McLaren na Williams zilikuwa za kwanza kukubali kusaini mkataba mpya na sasa wameungwa mkono na timu zingine zote. Mercedes ambao walikuwa wakihitaji maelezo zaidi kuhusu mkataba huu, nao sasa wameungana na wenzao na kusaini mkataba.

Taarifa ya F1 na FIA iliyotolewa leo inasema “makubaliano haya yatalinda maendeleo ya F1 pamoja na kuendana na masharti mapya yaliyotangazwa mwaka 2019 na yatatumika mwaka 2022. Pia yatapunguza tofauti kubwa ya mapato ya timu zinazoshiriki ili kusaidia kuwa na uwiano kwenye mchezo na kuwa na mchezo wa kuvutia mashabiki.”
F1 waliweka mwezi Agosti kuwa mwisho wa kusaini mkataba wa Concord Agreement.
Mwenyekiti wa Formula One – Chase Corey “Mwanzoni mwa mwaka tulisema, kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona, tutaongeza muda wa majadiliano na makubaliano ya Mkataba wa Concord Agreement. Tunafurahi kufikia Agosti, tumefanikiwa kukubaliana na timu zote 10.”
Raisi wa FIA – Jean Todt akaongeza kuwa, “kuhitimishwa kwa makubaliano kati ya FIA, F1 na timu zote 10 kunalinda maendeleo yajayo ya FIA Formula One Championship“.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


Magdalena
mambo mazuri yaja tunayasubiri kwa hamu
Latifa juma mohamed
Mambo yanazidi kutaradi kwa hamu tunayasubir
Sabrina
Bora turudi mchezoni
farida ahmadi
Habari nzuri Sana kwetu mashabiki
Samiah
Bora turud
Nasra
Turudi mchezoni tu
rama
Maoni:vizuri kama wamekubiliana vyema
Lydia Emmanuel Magoti
Habari nzuri kwa sisi mashabiki
Furahav
Jambo jema.
Tatu
Nilikuwa nasubili kwa hamu
Gabriel
Formula 1 iko poa sana tunatumain na makampun meng ya magar yatashirik
Povel
Mambo ni moto