Baada ya kupata maambukizi ya virusi vya COVID19, nafasi ya Lewis Hamilton kwenye timu ya Mercedes itazibwa na kijana – George Russell.

George Russell ni dereva wa timu ya Williams lakini Mercedes walikuwa wakimuongoza toka mwaka 2017 na alikuwa dereva wa ziada mwaka 2018 kabla ya timu hiyo (Mercedes) kumuachia ajiunge na Williams kwa mkataba wa miaka 3 kuanzia 2019.

George Russell ambaye anamiaka 22 pekee, anakwenda kuziba nafasi iliyoachwa na bingwa mara 7 wa Formula 1 – Lewis Hamilton ambaye atakosekana kwenye mbio za Sakhir Grand Prix wikiendi hii kutokana na maambukizi ya COVID19.

Akizungumza baada ya kupatiwa jukumu hili, Russell amesema “Nitakuwa nimevaa jezi ya timu nyingine wikiendi hii lakini mimi ni dereva wa Williams na nitakuwa nikiishangilia timu yangu kwenye kila hatua.

George Russell, George Russell Kuziba Nafasi ya Hamilton., Meridianbet
George Russell.

“Ninaiona hii kama nafasi kubwa ya kujifunza kutoka kwenye timu kubwa kwenye mchezo kwa sasa na nitarejea kama dereva aliyeongeza kiwango na mwenye uwezo mkubwa wa kuisaidia Williams kuendelea kusonga mbele. Niwashukuru sana Mercedes kwa kuniamini.

“Uhalisia ni kwamba hakuna wa kuchukua nafasi ya Lewis, lakini nitajitoa kwa uwezo wangu wote katika kuziba nafasi yake kuanzia nitakapoingia kwenye gari. Cha muhimu zaidi, ninamtakia afya njema apone haraka. ”

Mkurugenzi wa Mercedes – Toto Wolff amesema ” George ameonesha kiwango kikubwa msimu huu akiwa na Williams, alikuwa na mchango mkubwa katika kuipandisha timu hiyo kwenye nafasi za juu.

“Ninaamini atafanya vizuri akisaidiana na Valtteri [Bottas] ambaye atakuwa ni mfano mzuri kwake. Mbio hizi zitatupa picha nyingine ambapo tutamuona kijana aliyetengenezwa kwenye mikono yetu akiwaanaitumikia timu ya Mercedes kwa mara ya kwanza.”


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

George Russell, George Russell Kuziba Nafasi ya Hamilton., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

7 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa