Hakika mbio za Formula 1 msimu huu ni vita kubwa! Lewis Hamilton vs Max Verstappen, kwa mara ya nne msimu huu mwendo wao ni tairi kwa tairi msimu huu.

Pengine huu ni msimu ambao upinzani umekuwa wa karibu zaidi ikilinganishwa na mwaka 2018 ambapo, Mercedes walikuwa wakichuana na Ferrari ambao walikua na gari lenye mbio zaidi. Licha ya ubora wa Ferrari, Hamilton bado alionesha umwamba wake na kuibuka kinara.

Safari hii, Lewis Hamilton ameibuka na taji la Spanish GP likiwa ni taji lake la 2 tangu kuanza kwa msimu huu. Dereva huyu wa Mercedes, ameendelea kuwa bora msimu huu ambao anapata upinzani mkubwa kutoka kwa Max Verstappen kutoka timu ya Red Bull.

Hili ni taji la 98 kwa Lewis kwenye historia yake ya mchezo wa langalanga na anahitaji makombe mawili tu kukamilisha idadi kubwa ya mataji kwenye mchezo huo.

Hamilton, Hamilton Bingwa Wa Spanish GP., Meridianbet
Lewis Hamilton alimpiku Max Verstappen ikiwa imesalia mizunguko 6.

“Kila mwaka ninavyorudi, ninajitahidi kuongeza ubora. Kila mara inaonekana haiwezekani lakini ni lazima. 

Red Bull wameanza msimu vizuri. Wanagari zuri ambalo linaweza kuwapa ubingwa, kama sisi. Hii itatuhitaji kufanya kila tunaloweza, sio mimi tu kuonesha ubora wangu lakini na timu yangu kuonesha ubora wao, kila wikiendi. Tofauti na hapo, Red Bull watakuwa washindi” alisema Lewis Hamilton.

Sambamba na ushindi wa Lewis, imeripotiwa kuwa dereva huyo anahitaji kusaini mkataba mpya na timu ya Mercedes kabla ya majira ya joto kuanza msimu huu.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Hamilton, Hamilton Bingwa Wa Spanish GP., Meridianbet

CHEZA HAPA

5 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa