Habari mbaya kwa wapenzi wa mbio za magari ya Formula 1 (F1), bingwa wa dunia – Lewis Hamilton amekutwa na maambukizi ya COVID19 na atakosa mbio za Sakhir GP wikiendi hii.

Taarifa hii imeripotiwa baada ya timu ya Mercedes kuripoti kuwa Lewis Hamilton alianza kuonesha dalili za mgonjwa wa COVID19 na baada ya kufanyiwa vipimo mara mbili, matokeo yalionesha ameathirika.

Kwa sababu hiyo, Hamilton ameshajitenga na timu yake. Siku ya Jumapili, Hamilton alishinda mbio za 11 kwa mwaka huu baada ya kuibuka kidedea kwenye mbio za Bahrain Grand Prix.

Lewis Hamilton, Lewis Hamilton Kuikosa Sakhir GP., Meridianbet
Hamilton baada ya kushinda mbio za Bahrain Grand Prix wikiendi iliyopita.

Taarifa rasmi kutoka Mercedes imeandikwa “Mbali na kuonesha dalili, [Hamilton] yupo vizuri na timu nzima inamtumia salamu za kumtakia afya njema”

Mercedes bado hawajamtaja dereva atakayeziba pengo la Hamilton kwenye mbio za Sakhir GP wikiendi hii na wamesema mchakato huo utafanyika muda wowote kuanzia sasa.

Kukosekana kwenye mbio za Sakhir GP itakuwa ni mara ya kwanza kwa Lewis Hamilton kukosekana uwanjani tangu alipoanza kucheza F1 mwaka 2007.


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Lewis Hamilton, Lewis Hamilton Kuikosa Sakhir GP., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

15 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa