Nyota wa timu ya Mercedes Lewis Hamilton amekuwa kimya kwa muda mrefu tokea kumalizika kwa mashindano ya mwisho mwaka jana disemba jijini Abu Dhabi ambapo kulitokea sintofahamu nyingi kwenye mashindano hayo.
Hivi karubuni FIA walimtangaza kiongozi mpya wa taasisi hiyo bwana Mohammed Ben Sulayem kuchukua nafasi ya Jean Todt, ambapo alisisitiza kuwa Lewis Hamilton inabidi arudi mwaka 2022 ili aje kupambana na Verstappen.
Kiongozi mpya wa FIA Mohammed Ben Sulayem anauhakika kuwa Lewis Hamilton atarejea kwenye mbio hizo mwaka huu, japokuwa kuna tetesi zinazosambaa kuwa Lewis ana mapango wa kustaafu mbio hizo na kujikita zaidi kwenye maswala ya muziki na mitindo, huku aki unfollowed watu wote kwenye mtandao wa Instagram
“Hapana sifikilii hivyo, ni tetesi tu, kwani yeye mwenyewe ametangaza kustaafu? hapana. Lewis ni mtu muhimu kwenye sehemu ya mafanikio ya mchezo huu.” Alisema Mohammed
Mohammed Ben Sulayem amekubali kuwa amekuwa akisumbuka kufanya mawasiliano nae tokea sintofahamu ya jijini abu dhabi.
“Nilimtumia message, ndio, nadhani hayuko sawa kuweza kujibu naelewa nafasi yake, kuna sheria inabidi zifwate na madereva wote. Kwangu hakuna timu au dereva yeyote ambae yuko juu ya sheria za FIA.” Aliongezea
Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.