Bingwa mara saba wa mashindano ya F1 Lewis Hamilton amefichua siri kuwa anampango wa kubadili jina lake la koo na kuongeza jina la mama yake kwenye jina la ukoo.
Lewis Hamilton alimwalika mama yake kumwangalia akipokea “knighthood” kutoka kwa mwana mfalme Charles kwenye kasri ya Windsor mwezi December, pia amesema nia yake ya kujumuisha jina la mama yake, Larbalestier likiwa pamoja na Hamilton.

Hamilton wazazi wake kati ya mama yake na baba yake walitengana wakati akiwa na miaka miwili, akizungumza kwenye maandalizi ya msimu mpya wa F1 ambao unatarajiwa kuanza nchini Bahrain siku ya jumapili alinukuliwa alisema, “kiukweli najivunia jina la mama yangu.
“Jina la mama yangu ni Larbalestier na nakwenda kuliweka kwenye jina langu. Sielewi kwa nini watu wanapoana mwanamke anapoteza jina lake na kiukweli nataka jina la mama yangu liwe sambamba na jina la Hamilton.”
Alipoulizwa lini anatarajia kubadilisha jina Hamilton alijibu, “natumai hivi karibuni, Tunalifanyia kazi sasa.”
Lewis Hamilton sasa anafanya maadalizi y kushiriki kwenye msimu wa wake wa 16 ili kuweza kulipa kisasi cha msimu uliopita baada ya matokeao ya mwisho kuwa na utata na Max Verstappen kutangazwa mshindi wa mashindano hayo.
SHAOLIN FORTUNES 100 ONJA LADHA YA USHINDI
Maana ya ushindi mkubwa ipo hapa katika mchezo wa SHAOLIN FORTUNES 100 ndani ya kasino maridhawa za meridianbettz. Kwa dau dogo unashinda zaidi, unaweza kucheza mara nyingi uwezavyo huku ukifurahia ladha ya ushindi.