Klabu ya Sevilla imemtangaza rasmi Luis Garcia Plaza kuwa kocha mkuu mpya, siku moja tu baada ya kumfuta kazi aliyekuwa kocha wao Matias Almeyda kufuatia matokeo yasiyoridhisha ndani ya La Liga.
Kupitia taarifa rasmi, Sevilla ilithibitisha kufikiwa kwa makubaliano na kocha huyo mzaliwa wa Madrid, ambaye atasimamia timu hiyo hadi Juni 30, 2027. “Sevilla FC imefikia makubaliano na kocha Luis Garcia Plaza, ambaye atachukua jukumu la kuinoa timu ya kwanza hadi Juni 2027,” ilisema taarifa ya klabu hiyo.
Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa
Sevilla kwa sasa inapitia kipindi kigumu, ikiwa nafasi ya 15 kwenye msimamo wa La Liga, ikiwa ni alama tatu tu juu ya eneo la kushuka daraja, hali inayolazimisha mabadiliko ya haraka ya kiufundi.
Garcia Plaza mwenye umri wa miaka 53 ana uzoefu mkubwa wa La Liga, akiwa amesimamia jumla ya michezo 229 akiwa na klabu mbalimbali zikiwemo Levante UD, Getafe CF, Villarreal CF pamoja na Deportivo Alavés, ingawa aliachishwa kazi Alavés mwezi Desemba 2024.
Kocha aliyefukuzwa, Almeyda, alisimamia mechi 32 za mashindano yote msimu huu, lakini aliondolewa baada ya kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Valencia CF kilichoiacha Sevilla kwenye hatari ya kushuka daraja.
Licha ya ukame wa mataji ya ndani tangu walipotwaa Copa del Rey mwaka 2010, Sevilla imeendelea kung’ara kimataifa kwa kushinda taji la UEFA Europa League mara saba tangu mwaka 2006, ikiwa ni moja ya klabu zenye mafanikio makubwa katika mashindano hayo barani Ulaya.

