Yuki Tsunoda Ajiunga na Timu ya Alpha Tauri.

Kuelekea msimu mpya wa Formula 1, mchezaji chipukizi Yuki Tsunoda amejiunga na timu ya Alpha Tauri. Sasa ni rasmi kijana huyu atashiriki Formula 1 msimu ujao.

Tsunoda alimaliza katika nafasi ya 3 kwenye mbio za Formula 2 akiwa na timu ya Red Bull ambayo ilikuwa ikifanya kazi na Honda kama washirika wao.

Kiongozi wa Alpha Tauri – Franz Tost amesema ” Mwaka huu kwenye F2, Yuki Tsunoda ameonesha mchanganyiko mzuri wa namna ya uendeshaji pamoja na uelewa mkubwa wa masuala ya kiufundi. 

Tsunoda baada ya kumaliza katika nafasi ya 3 kwenye mbio za Formula 2.

“Ninahakika atakuwa na mchango mkubwa kwenye timu yetu. Kwenye mbio 2 za majaribio (Imola na Yas Marina), amethibitisha yupo tayari kucheza Formula 1.”

Hii ni hatua kubwa kwa mchezaji chipukizi kama Tsunoda ambaye ni kijana wa miaka 20 pekee. Kwa Tsunoda ” kama ilivyo kwa madereva wengine, lilikuwa ni lengo langu kucheza Formula 1, nimefurahi sana kwa taarifa hii.

“Nimegundua nitakuwa nimebeba matumaini ya wajapani wengi ambao ni mashabiki wa F1 na nitajitahidi kuwapafuraha.”

Tsunoda alipokuwa uwanjani na timu ya Red Bull.

Yuki Tsunoda anakuwa Mjapani wa kwanza kucheza F1 baada ya Kamui Kobayashi ambaye aliipeperusha bendera ya timu ya Toyota kwenye mbio mbili za mwishoni mwaka 2019.

Sauber na Caterham ni wajapani wengine ambao waliwahi kucheza mashindano ya Formula 1 katika historia ya mashindano hayo.


BURUDIKA NA WANYAMAPORI WAKIIMBA NA KUPIGA VYOMBO VYA MUZIKI!

Kupitia Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet, furahia mchezo wa Forest Rock. Hapa utaburudika na umahiri wa wanyapori wanaoimba na kutumia vifaa vya muziki wa rock. Burudika huku ukijiwekea nafasi ya kutengeneza pesa ndefu kupitia Meridianbet!!

INGIA MCHEZONI!

18 Komentara

    All ze best kijana

    Jibu

    Kila lakheri yuki majukumu yanaendelea

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Dereva bora

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Kila la kheri

    Jibu

    Dereva bora

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    Habari njema kwa mashabk

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Vizuri sana

    Jibu

    All the best kwako

    Jibu

    Kila lakheri

    Jibu

    Safi sanaaa

    Jibu

    kila la kheri

    Jibu

    Kila la khery

    Jibu

    Safi

    Jibu

    Yuki ni mda alikuwa anatamani kujiunga na hii timu

    Jibu

Acha ujumbe