Rio Fredinand anaamini kuwa bado Liverpool wana nafasi ya kumaliza nafasi ya nne na kucheza michuano ya UEFA msimu ujao.

Ligi kuu ya Uingereza inaelekea ukingoni na bado kuna vita kubwa sana ya kuwania nafasi nne za juu ili kucheza klabu bingwa ulaya msimu ujao. Baada ya City kuwa mabingwa, Manchester United kushika nafasi ya Pili. Vita iliyobaki ni nafasi ya tatu na ya nne ambayo itamalizwa na michezo iliyobaki.

Timu ya Chelsea iliibuka na ushindi hapo jana dhidi ya Leicester City na kujisogeza mpaka nafasi ya 3 wakiwa na alama 67 juu ya Leicester wenye alama 66 wakati huo huo Liverpool wana alama 63 wakiwa na mchezo mmoja mkononi.

Liverpool watakuwa dimbani leo kupambana na Burnley na ushindi wa mechi hii utawapeleka mpaka nafasi ya 4 wakimpita Leicester kwa magoli ya kuufunga na kufungwa.

Fredinand anaamini kuwa Liverpool wamekuwa wakicheza kwa kujitolea sana mechi hizi za mwisho, huku akioneshwa kufurahishwa na goli zuri alilofunga kipa wa Liverpool juzi kwa kichwa. Kwa kuelezea kuwa goli lilikuwa muhimu sana kwa Liverpool na anafurahi kuona kipa anafanya kitu cha kusaidia timu kama kile.
Fredinand on Liverpool1
Wachezaji wa Liverpool wakishangilia goli la Kipa wao lililowapa ushindi dakika za mwisho

Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United Fredinand anaamini kuwa vijana wa Klopp wanaweza kumaliza nafasi nne za juu na kufuzu kuchezea ligi ya mabingwa ulaya msimu huu, endapo watashinda mechi ya Leo dhidi ya Burnley.


UNAWEZA KUWA MILIONEA WAKATI WOWOTE!

Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.

FREDINAND, Fredinand: Liverpool watamaliza Top 4 Msimu hUU, MeridianbetBASHIRI SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa