Nyota wa Barcelona Frenkie de Jong ameonya kuwa Barcelona inaenda kuwa timu bora sana msimu huu licha ya sakata la kiuchumi linaloikumba klabu hiyo.

Ishu kubwa inayotawala vicha vya habari juu ya Barcelona kwa sasa ni suala la fedha na kushindwa kwao kukamilisha usajili wa Lionel Messi mpaka sasa. Lakini de Jong bado ana matumaini kuwa wapo kwenye njia sahihi.

Licha ya sakata la kushindwa kukamilisha usajili wa Messi, kocha Ronald Koeman amepata kikosi chenye wachezaji wazuri na wenye vipaji kuelekea msimu mpya, wakiwemo Sergio Aguero, Memphis Depay, Eric Garcia na Emerson Royal kwenye sehemu ya kikosi hicho.

Frenkie De Jong
Frenkie De Jong

Licha ya masuala ya nje ya uwanja, Barcelona watahitaji kufanya kila liwezekanalo kujiboresha zaidi msimu huu. Na Frenkie de Jong anasema;

“Ninaamini kikosi kitakuwa bora zaidi kwenye msimu huu wa joto, tunaenda kuwa bora zaidi kama timu. Ni mwaka wa pili wa bosi (Ronald Koeman) ni kawaida kuwa bora kwenye mwaka wa pili. Ninadhani tutapata fursa ya kupambana na kushinda mataji muhimu msimu unaokuja.”

 

Frenkie de Jong


VUNA MKWANJA NA KASINO ZA MERIDIANBET!

Unakila sababu ya kuwa moja ya mamilionea katika kasino za mtandaoni za meridianbettz, Mchezo wa Ruby Casino Queen unaweza kukufanya ujishindie mkwanja mrefu. Furahia ubora wa kasino zetu na njia kibao za kuwa mshindi leo hii ukiwa na mrembo Ruby.!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa