Mchezaji wa Liverpool, Harry Wilson amekamilisha uhamisho na kujiunga na Fulham, baada ya miaka 16 katika klabu hiyo tangu alipojiunga nao akiwa na miaka 9.

Wilson alianza kuitwa timu ya taifa akiwa na umri wa miaka 16 mnamo 2013 na baadaye akafanya vizuri Liverpool U23s huku akivutia vilabu vingi kutokana na uwezo wake kwenye mpira, kufunga na kupiga mashuti.

Alionekana katika kikosi cha kwanza kwa Reds kama mbadala katika mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Plymouth Argyle mnamo Januari 2017, kabla ya kutolewa kwa mkopo.

Akiwa na Hull City na kisha Derby County, Wilson akifunga mabao 23 kwenye mashindano, na baadaye msimu wa 2019-20 alijiunga na AFC Bournemouth kwenye Ligi ya Premia.

Aliporudi Liverpool, alicheza mechi yake ya pili ya wakubwa chini ya Jürgen Klopp na kuanza dhidi ya Arsenal kwenye Kombe la Ligi Oktoba iliyopita.

Wilson aliondoka kwa mkopo tena, na kujiunga na Cardiff City kwenye ligi daraja la pili la mpira wa miguu la Uingereza, ambapo alifunga magoli saba kabla ya kujiunga na Fulham msimu huu baada ya kutoka katika mashindano ya Euro 2020.

Fulham wameshuka daraja katika ligi kuu ya EPL msimu uliopita na watacheza Championship katika msimu ujao wa 2021/2022.


FURAHIA KASINO MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

2 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa