Ole Gunnar ameanza kuingiwa na wasiwasi mkubwa ndani ya kikosi chake cha Ujited mara baada ya kupungua kwa mwahusiano mazuri na baadhi ya nyota wa kikosi hicho ambao wanaona kwa upande fulani kama mbinu za kocha hiyo zimeshindwa kabisa kutafuta matokeo. Mbali na kuonekana kuna baadhi ya watu wanamkingia kifua lakini kuna walakini endapo ataendelea kuhudumu kutokana na aina ya matokeo ambayo kikosi chake hicho kimekuwa kikiyapokea jambo ambalo haliwezi kuvumilika kulingana na shinikizo litakalotolewa na mashabiki juu ya kuchoka kwao na mwenendo wa kikosi hicho.

Ikiwa kama sehemu ya makubaliano baada ya usajili wa kiungo wa kikosi cha Barcelona ambaye aliichezea klabu ya majogoo hao wa jiji la Uingereza na kwa sasa akiwa anahudumu kwa mkopo ndani ya klabu ya Bayern Munich sasa huenda Majogoo hao wakaanza kula kitita cha £4.5M kutoka kwenye biashara ya Coutinho kwenye kile kitita cha £84M ambazo zilikuwa kama malipo ya nyota huyo baada ya kuihama Liverpool.

Everton wapo mbioni kuingilia dili la United juu ya usajili wa nyota, Moussa Dembele ambaye amekuwa akifukuziwa na klabu hiyo kwa kipindi kirefu. Everton wanatamani sana kumnasa mchezaji huyo ili kuweza kukipa nguvu endapo nyota huyo ataendelea kuwa katika mipango ya walimu watakaotua ndani ya kikosi hicho.

Nyota wa klabu ya Chelsea ambaye amejiunga na klabu hiyo kutoka Borussia kwa uhamisho wa ada ya £58M, Pulisic anaonekana kuanza kuchukizwa na maisha ya klabuni hapo mara baada ya kuanza kukosa muda wa kucheza. Hiyo ni baada ya kuwa kikosini hapo kwa muda lakini nafasi yake inaonekana kuwa finyu sana jambo ambalo linaonekana kumfanya akumbuke sana maisha yake ya ujerumani ambako alikuwa na namba ya kudumu.

Ndoto ya kocha wa klabu ya Crystal Palace, Roy Hodgson ni kuifanya klabu yake inamaliza katika nafasi sita za juu mara baada ya kuona kinachofanywa na wachezaji wake kina kila dalili ya kuweza kuwafikisha huko. Hadi sasa anaangalia jukumu la kuweza kufanya usajili ndani ya kikosi chake hususani katika nafasi ya mshambuliaji ili kuongeza makali zaidi ndani ya kikosi hicho.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa