Taarifa zinazidi kutembea kwamba klabu ya Juventus iko mbioni kuwataka nyota wa Manchester United mbali na kwamba wanaweza kukutana na ushindani mkubwa katika kumnasa mlinda mlango huyo. Juventus wameweka njia ya kutaka kumsajili De Gea katika dirisha la majira ya joto ili aweze kutua kikosini hapo. Mbalj na De Gea pia wanaangalia namna wanavyoweza kuwanasa nyota wengine wawili ambao ni Baily na Matic.

Jitihada za klabu ya Tottenham kutaka kumnasa Bruno Fernandes raia wa Ureno ziligonga mwamba mara baada ya kuwepo kwa baadhi ya pingamizi ambazo ni za kiusajili kwa nyota huyo ambaye kuna baadhi ya taratibu zilikuwa ni vigumu kufikiwa kwa kipindi kifupi kama kile. Jambo hilo lilipelekea ugumu. Baadhi ya mambo yaliyokuwepo ni malipo kwa baadhi ya ubingwa ambao Spurs wangechukua walitakiwa kugawana faida kidogo.

Samuel Chukwueze ni miongoni mwa kinda wanaofanya vizuri sana katika klabu ya Villareal. Nyota huyo kwa sasa anaonekana kuwindwa sana hata sokoni kutokana na ubora wake. Liverpool wameweka wazi kwamba wanahitaji kuona nyota huyo akitua katika viunga vyake ili kusaidia timu yao.

Callum Husdon-Odoi, nyota anayekipiga na klabu ya Chelsea, anaangalia uwezekano wake wa kuongeza kandarasi ya kuendelea kuwatumikia Wanadarajani hao mbali na kwamba hajapata muda mwingi wa kuweza kucheza na kikosi hicho. Nyota huyo hajawa chaguo la kudumu la Lampard jambo ambalo linampa wakati mgumu kikosini hapo.

Klabu ya Aston Villa ya Uingereza imeweka mezani dau lake la kutaka kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Celta Virgo, Pione Sisto (24). Nyota huyo mwenye kiwango cha pekee huenda akajiunga na klabu hiyo katika msimu huu wa joto kwenye harakati za kutafuta namba ya kudumu na mahala ambapo pataweza kumfaa zaidi.

Mchezaji wa Leicester City, James Maddison anaangalia juu ya maisha yake ndani ya klabu hiyo huku tayari akianza kuhusishwa na kujiunga na klabu ya Manchester United ambao wanaonekana kuvutiwa sana na nyota huyo.

Inaonekana kwamba klabu ya Real Madrid hawakuwa na uzito sana juu ya usajili wa Neymar na dili lao kubwa lilikuwa ni kuwatisha Barcelona kwamba wanao uwezo na maamuzi ya kumsajili nyota yeyote wanayeamua kufanya naye kazi ila baadaye klabu zote mbili zilishindwa kumnasa nyota huyo wa taifa la Brazil na klabu ya PSG.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa