Wakala wa mshambuliaji wa pembeni wa Real Madrid, Gareth Bale amesema mchezaji wake anataka aendelee kubakia klabuni hapo, na sio kurudi EPL. Bale amekuwa anahusishwa na mpango wa kurejea katika ligi ya England (EPL) huku klabu yake ya zamani Tottenham Hotspur na Manchester United zikitajwa kuiwinda saini yake.
, Gareth Bale Hatorudi EPL Anafurahia Maisha ya Real Madrid, Meridianbet
Gareth Bale
Winga huyo raia wa Wales mwenye miaka 30, siku za hivi karibuni alikuwa anahusishwa kurudi EPL baada ya kutokuwa kwenye maelewano mazuri na kocha wake, Zinedine Zidane. Bale ilibakia kidogo tu ajiunge na timu mojawapo ya China msimu uliopita baada ya sintofahamu ndani ya klabu ya mabingwa mara nyingi zaidi wa ligi ya mabingwa Ulaya (UEFA – 13).
Akizungumzia kuhusiana na tetesi hizo amesema “Sifikirii kama hilo linaweza kutokea kipindi hiki, licha ya kushinda karibia kila timu Madrid bado anaonekana kuwa na furaha,” alisema Jonathan Barnett (wakala wa Bale).
, Gareth Bale Hatorudi EPL Anafurahia Maisha ya Real Madrid, Meridianbet
Gareth-Bale
“Kurudi EPL itakuwa ni jambo kubwa kwa sababu ya aina ya maisha anayoishi hapa, hana tamaa ya fedha kama wengine hivyo sioni kama hilo linaweza kutokea,” aliongeza. Tangu ajiunge na Real Madrid kwa rekodi ya aina yake mwaka 2013, Gareth Bale ameshinda mataji kama ligi ya mabingwa mara nne, La Liga, Copa del Rey, Kombe la Dunia ngazi ya vilabu, na Kombe la ligi ya Hispania yote mara moja, na Uefa Super mara tatu.

41 MAONI

  1. Abaki la liga kwn epl hakuna timu ambayo inawezah kumlipa mshahara kwa janga hl la korona thnks meridian bet kwa update

  2. Wakala Jonathan Barnett anachokizungumza yuko sahihi na ukiangalia bale n mchezaji mzur then anazid kuelezea n mchezaji ambaye anamapenz na timu sio anatamaa na hela

  3. Bale ilibakia kidogo tu ajiunge na timu mojawapo ya China msimu uliopita baada ya sintofahamu ndani ya klabu ya mabingwa sasa afanye mambo sio alegeze

  4. Bale ametoa mchango mdogo sana Real Madrid na amekuwa na kiwango cha chini tofauti na alivyokuwa Tottenham. Auzwe tu!#meridianbettz

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa