Genoa Italia, klabu kongwe kotoka Italia na imayokuwa kwa kasi katika ligi kuu ya Italia imeuzwa kwa kampuni inayotoka Amerika ya Kaskazini.

Genoa iliyoanzishwa mwaka 1893, imeuzwa kwa kampuni binafsi kutoka Marekani inayojulikana kama 777 Partners, klabu imetangaza kuwa 777 partenrs wamelipa kiasi cha $175 millioni, huku akichukua hisa asilimia 99.9 ya hisa zote.

Genoa

Klabu ilitoa waraka uliondikwa, “mmiliki wa awali, Enrico Preziosi, atabaki kwenye bodi ya wakurugenzi, wakati mkurugenzi mwendeshaji ataendelea na kazi zake za kila siku klabuni.”

Preziosi ambaye ameimiliki klabu kwa miaka 18, alisema “muda umefika sasa, kama nilivyokuwa nasema kwamba, kama nitaondoka, basi sina budi kuicha Genoa kwa mtu imara.”

Ujumbe wa wawekezaji uliongozwa na Josh Wander na Steve Pasko, waanzilshi wa 777 Partners, pia alikuwepo Juan Arciniegas, ambaye anasimamia maswala yote ya michezo na burudani, akiambatana na meneja mwendeshaji wa michezo na uwekezaji Andres Blazquez.

Genoa inaungana na timu sita nyingine za serie A zinazomilikiwa na wamerekani AC Milan, Roma, Fiorentina, Bologna, Spezia na Venezia.


FUNGA BAHATI YAKO NA MERIDIANBET.

Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa