Kiungo wa Chelsea na Scotland, Billy Gilmour atajitenga kwa siku 10 baada ya kupimwa na kukutwa na maambukizi ya Covid-19 na atakosa mchezo wa mwisho wa makundi wa Euro 2020 dhidi ya Croatia siku ya Jumanne.

Gilmour, 20 alicheza dakika zote kwa mara ya kwanza katika mechi yake ya kimataifa dhidi ya England Ijumaa, alikuwa mchezaji bora wa mechi wakati Scotland ikitoka sare isiyo na magoli huko Wembley.

 

gilmour, Gilmour Akutwa na Maambukizi ya Covid-19., Meridianbet

“FA ya Scotland inadhibitisha kwamba mchezaji wa kikosi cha wachezaji wa timu ya taifa ya Scotland, Billy Gilmour, amepimwa na kukutwa na maambukizi ya Covid-19,” SFA ilisema katika taarifa.

 

“Baada ya kuwasiliana na wataalam wa Afya ya Umma England tangu matokeo hayo yarekodiwe, Gilmour sasa atajitenga kwa siku 10 na kwa hivyo atakosa mechi ya kesho ya Kundi D la UEFA EURO 2020 dhidi ya Croatia huko Hampden.”

Mchezaji huyo hatakuwepo kwa mchezo wao muhimu dhidi ya Croatia huko Hampden Park na pia uwezekano wa mechi ya raundi ya 16 iwapo Scotland itafuzu kwa hatua ya mtoano ya mashindano makubwa kwa mara ya kwanza.

Hakuna wachezaji wengine waliobainika kuathiriwa au kutambuliwa hata wale wenye mawasiliano ya karibu na mchezaji huyo, kama wamepata maambukizi, hivyo kikosi kilichosalia chote kitakuwa tayari kwajili ya mchezo unaofuata.


USHINDI BILA MIPAKA!

Hakuna mipaka ya ushindi kwenye Keno Instant ya meridianbet Kasino, hii wewe ndiyo una uamuzi zaidi juu ya mchezo na nafasi ya machaguo kibao.
Arsenal, Arsenal Wawasilisha Ofa ya Pili Joaquin Correa., Meridianbet

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa